Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
Mh. Jenista Mhagama Mbunge wa jimbo la Peramiho mara baada ya kupokelewa
katika eneo la Seminari Kuu Peramiho akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi na kukagua
miradi ya maendeleo na kuimarisha uhai wa chama Songea mkoani
Ruvuma.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-PERAMIHO
Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akisalimiana na
Mh. Jenista Mhagama Mbunge wa jimbo la Peramiho mara baada ya
kupokelewa katika kijiji cha Seminari kuu Peramiho , katikati ni Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole
na Julius John Kiongozi wa kimila mara baada ya kuwasili Peramiho Leo
kwa ziara ya kikazi.kulia ni Oddo Mrisho Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Ruvuma na kulia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea silaha za
kijadi kutoka kwa Julius John Kiongozi wa kimila kama ishara ya
kuogoza na kusimamia vyema chama ili kiwe imara zaidi mara baada ya
kuwasili Peramiho Leo kwa ziara ya kikazi
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
wanachama katika shina namba 28 wakati alipomtembelea balozi Said Issa
mara baada ya kuwasili Peramiho Leo kwa ziara ya kikazi
Mbunge
wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akiwa amekaa kwenye mkeka na
wana CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
balozi wa shina namba 28 Ndugu Said Issa huku wakinywa chai wakati
alipomtembelea nyumbani kwake kulia anayewasikiliza ni Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama. Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza
Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh Jenista Mhagama huku wainywa chai
katikati ni Balozi wa shina namba 28 Bw. Said Issa, kulia ni Mkuu wa
mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa Dr. Asha Rose Migiro na Mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Ruvuma Bw. Oddo Mrisho.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza kabla ya katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzungumza na viongozi wa mashina katika mkutano wa ndani mjini Peramiho.
Nape Nnauye akipiga gitaa huku mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama kulia akicheza.


ongera sana mi naomba kuwa mwandhi wa hii blog yako tarifa zako kama nafasi ipo
JibuFutanamba yangu 0659503616