Nilimfahamu muda mrefu tangu akiwa kama mwalimu pale Peramiho Girls.
Kukurukakara zake za kupigania haki za walimu kuanzia alipokuwa mwalimu,
kisha UWT hadi kuwa mbunge wa Peramiho, zimeonekana kwa kiasi kikubwa,
hata sasa kuteuliwa kuchukua nafasi ya Phillip Mulugo kama Naibu Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Tanzania.
Kuteuliwa kwake katika nafasi hii kumenipa faraja kwa kuwa utekelezwaji
wa mpango wa "Matokeo Makubwa Sasa' katika sekta ya elimu unaweza
ukaangaliwa kwa jicho la uzoefu zaidi katika kuhakikisha kwamba walimu
wanapewa haki zao kama inavyotakiwa kwa kuwa Mheshimiwa Jenista Mhagama
naye amepitia njia hiyo hiyo.
Pia, sote tunafahamu misimamo yake mikali awapo bungeni hasa katika
utekelezaji wa mikakati yenye manufaa kwa wananchi. Nina imani kubwa
kuwa Wizara ya Elimu haitakuwa kama ilivyokuwa kwa miaka yote ya nyuma.
Jambo moja tu ambalo nadhani mheshimiwa Rais JK angeliangalia kwa jicho
la ziada, ni kwamba Wizara nzima ingevunjwa na mfumo wake ujengwe upya,
kuanzia Waziri Dkt shukuru Kawambwa mpaka makatibu wa Wizara na
watendaji wake ambao wamekaa Wizarani kwa muda mrefu bila kuwa na
matunda mazuri.
Nina imani uchapakazi wa mheshimiwa Jenista Mhagama utafunika udhaifu wa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi mheshimiwa Dkt Shukuru Kawambwa.
Weka maoni yako hapa!

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni